Tuesday, April 15, 2008
FROM HERE TO UDAKU PIPELINES
Wikiendi iliyopita moja ya magazeti maarufu kwa udaku Tanzania ( SANI) walichapisha habari kuhusu Mama mmoja mwenye asili ya kijapani jinsi alivyogoma kuruhusu gari lake lichukuliwe na jamaa wa City. Wadau kama mnakumbuka picha hizo hapo chini, zilipigwa na mdau Kylex kutumia Motorola kisha SIMUYANGUKAMERA ikaziposti. Mnasemaje wadau? Mimi sina noma wala nini since jamaa wamenipa shavu kwenye gazeti ( Wametaja source) its all good lets share the infoz with the good intentions.
Thursday, April 3, 2008
MWENDO WA KOMEO TU
PATAKUWA HAPATOSHI
Monday, March 31, 2008
MJAPANI AKOMAA KICHWA!

Mdau kylex kanitumia hizi kutoka kwenye Motorola yake. Ilikuwa leo mchana maeneo ya kisutu ambapo songombingo hili lilitokea.Mama watu kamshusha mtoto wake ile anarudi kupaki fresh anakuta Clamp!!Jamaa wa City walipiga Clamp baluni la Mjapani mida ya saa 7 mchana hivi, baadae wakarudi na Breakdown ili kusepa nalo mpaka kituoni.Walipofika wakamkuta mmiliki wa gari ambaye alikuwa mama mjamzito wa Kijapani amekaa juu ya gari hilo akiweka mgomo na kusema "mkilichukua gari hili basi na mimi pia mnichukue tutajua huko huko kituoni! KUDADADEKI!!" Kutokana na kupishana lugha ( Kijapani + English = Kiswahili not reachable) jamaa ikabidi wamuite boss wao aongee na Ninja huyo wa kijapani na baada ya maelezo ya kutosha ikabidi waiachie gari yake huru.
Sunday, March 30, 2008
MSAADA PLEASE
Mambo vipi wadau? I hope weekend haikuwa mbaya.Well, kuna mdau ana swali na anaomba tumsaidie maana ya neno "MALAVI DAVI" Kwa kuanza tu mimi ninavyojua Malavi davi ni MAPENZI sijui kama kuna maana nyingine, na nimeshalitumia neno hilo kwenye baadhi ya post haswa zinazohusu mizinga ( Ajali) za barabarani nikiambatanisha na neno kama KISS ambalo nalitumia kama neno MZINGA/ PASI/ KUGONGANA na kadhalika.Jamani wadau naomba tumsaidie mdau mwenzetu aliyeuliza kama ifuatavyo:
" malavi davi maana yake nini maana viswahili vya bongo bwana vigumu kweli kweli najua tu blog ya Dianah ndio inaitwa hivyo"
" malavi davi maana yake nini maana viswahili vya bongo bwana vigumu kweli kweli najua tu blog ya Dianah ndio inaitwa hivyo"
Friday, March 28, 2008
CHOKORAA!
Wednesday, March 26, 2008
IT RAINED CATS, DOGS, AND RATS!!!!!
Jana ilikuwa jua kaliii!!!!.Leo mvua kubwa imeshambulia jiji la DSM kuanzia mida ya saa sita 7 fulani mchana mpaka jioni ya saa 12.Mitaro,barabara na majengo mbalimbali yalifurikwa na maji, msongamano wa magari ndio usipimeeeee!!!! Kutoka Aga khani kuja posta masaa 2!!! Chukua hiyo!!
Wednesday, March 12, 2008
MORE ROAD DRAMAZ
Subscribe to:
Posts (Atom)














